Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Zainab Abdallah mapema leo tarehe 11/10/2024 ameongoza wananchi wa Kitongoji cha Mbaramo kwenye zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura
Zoezi hilo la kujiandikisha kwenye Orodha ya Wapiga Kura ni miongoni mwa maandalizi muhimu katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024, ambapo wananchi watapata nafasi ya kupiga kura na kuchagua viongozi wa Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji.
Mhe. Zainab amewataka wananchi wote kufika kwenye vituo vyakujiandikisha ambavyo vitakuwa wazi kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni, kuanzia leo tarehe 11 hadi tarehe 20 Oktoba 2024.
Ameendelea kuwasihi wananchi washiriki kwa wingi katika tukio hili muhimu kutakakopelekea kupata viongozi bora watakaowaletea maendeleo.
"Ndugu zangu wana Muheza tujitokeze kwenye kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura maana dakika yako moja utakayotumia kuja kujiandikisha itaamua mustakabali wa maendeleo ya eneo lako kwa kipindi cha miaka mitano ijayo’’ alisema Mhe. Zainab
Wananchi wamehimizwa kuendelea kutumia haki yao ya msingi yakikatiba kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha katika zoezi hili muhimu.
"SERIKALI ZA MITAA SAUTI YA WANANCHI JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI"
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.