Mkuu wa Wilaya Muheza Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo leo jumatatu tarehe 27/4/2020 amezindua kampeni ya kupambana na ugonjwa wa Corona Covid-19 iliofanyika nje ya ukumbi wa mikutano ya Halmashauri .
Akizungumza katika Uzinduzi huo Mhe Mwanasha amewataka wawezeshaji wakawaelimishe wananchi kupewa zawadi ya barakoa na mtu wasio mfahamu labda mtu huyo awe ni ndugu wa karibu ili kuepuka kutumia barakoa zilizowekewa dawa za kumdhuru binadamu.
Pia aliwataka waelimishaji kwenda kuwatoa hofu wananchi kwa kuwaeleza kuwa Serikali imejipanga kuhudumia wagonjwa watakaokuwa wamebainika kuwa na maambukizi kwani sio kila anaeumwa na kufa anakufa na Corona, kuna walougua corona na mpaka sasa wamepona.
Aliongeza kuwa elimu ikatolewe kwa wananchi kuhusu kuepukana na mikusanyiko kutoshikana mikono kikiwa ni tahadhari ya ugonjwa wa Corona , wanapokuwa kwenye vijiwe vya kahawa wahakikishe wanakaa umbali zaidi ya mita moja.
Vile vile aliwataka watoa Elimu wakaelimishe wananchi juu ya utumiaji wa lishe bora kwani hutengeneza kinga ya mwili ili kupambana na magonjwa .
Aidha amewataka wazazi kuwazua watoto wasizagae hovyo mitaani ikiwa ni kuwakinga na corona na ukatili wanaofanyiwa pindi wawapo mitaani.
“ Serikali imeamua kufunga Shule zote za Msingi, Sekondari na vyuo ili watoto wabaki nyumbani sio tu kuwakinga na ugonjwa wa Corona bali pia kuwakinga na vitendo viovu vya ubakaji na ulawiti, iwapo tutamkuta mtoto anadhurura mitaani hatua kali zitachukuliwa dhidi yako mzazi ulieshindwa kumsimamia” alisema Mhe, Mkuu wa Wilaya.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi( CCM) Mhe LAICKY GUGU aliwataka wananchi wote waliopo kwenye maeneo ya mikusanyiko kuvaa barakoa muda wote atakaeshindwa kutekeleza hili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Pia alisisitiza kuwa mtu yeyote atakaehisi dalili za ugonjwa huu afike kituo cha Afya kilichopo karibu nae kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ili kubaini tatizo linalomsumbua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Timu ya uhamasishaji dhidi ya Corona ambae ni Afisa Maendeleo ya jamii ya Rose Kimaro amesema Zoezi la utoaji Elimu Wilayani litachukua muda wa siku 19 kuanzia tarehe 27/4/2020 hadi tarehe 15/5/2020 ambapo zoezi hili litafanyika kwa kila kata nyumba kwa nyumba.
Aidha kampeni ya utoaji wa Elimu ya Corona inaongozwa na kauli mbiu isemayo "TATIZO CORONA, TAHADHARI IANZE NA WEWE". ikiwa na maana kuwa jukumu la kuchukua tahadhari ya Ugonjwa huu sio la mtu mmoja ni la kila mtu aliopo kwenye jamii husika.
MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA MUHEZA MHE, LAICKY GUGU AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZINDUZI. | MKUU WA WILAYA MHE, MWANASHA TUMBO AKIKABIDHI VITENDEA KAZI (BARAKOA) KWA WANAHAMASA | MKUU WA WILAYA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WANAHAMASA. | ||
|
||||
|
||||
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.