Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Halima Abdallah Bulembo amefungua Mafunzo ya ya siku 5 ya Mpango wa kunusuru kaya Maskini awamu ya tatu kipindi cha pili (TASAF) utakaowezesha kaya ambazo hazikuwemo kwenye mpango ziingizwe katika mpango huu..
Mkuu huyo wa Wilaya amesema Mpango wa awamu hii utahusisha vijiji 43 ambavyo havikuingizwa kwenye mpango uliopita ili walengwa wa kaya hizo waweze kunufaika kama ambavyo kaya za awali zinanufaika hali iliyopelekea malalamiko mengi kwa jamii na Taifa kwa ujumla
“waheshimiwa madiwani, washiriki wa mafunzo pamoja na wataalam wote tukasimamie vyema zoezi hili kila mmoja kwa nafasi yake ili tuweze kufanikisha jambo hili, tuhakikishe watu wanaoingia kwenye mpango huu ni wale wenye sifa kweli ili kupunguza malalamiko kwa wananchi” alisema Mhe. Bulembo.
Mafunzo hayo yalifanyika juzi tarehe 6/7/20211 katika ukumbi wa TATE PLUS na kuhudhuriwa na Waheshimiwa madiwani, wakuu wa idara, Timu ya wataalam kutoka TASAF makao makuu, Washiriki wa Mafunzo na Waandishi wa habari.
Awali akisoma hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu sehemu ya pili ya awamu ya tatu ya TASAF mtaalamu kutoka makao makuu Kelvin simon amesema tathmini ya utekelezaji wa kipindi cha kwanza cha Awamu ya tatu imeonyesha kwamba program hii imechangia katika kufikiwa kwa azma serikali ya kupunguza umaskini nchini.
Aliendelea kuwa takwimu zinaonyesha kwamba umaskini wa mahitaji ya msingi kwa kaya za walengwa umepungua kwa asilimia 10 na umaskini uliokithiri kwa kaya za walengwa umepungua kwa asilimia 12 hii imetokana na walengwa kujikita katika shughuli za kuuza kipato zikiwemo ufugaji, kilimo, uvuvi na kufanya miradi ya ujasiriamali.
Aliongeza kuwa, Kipindi cha Pili awamu ya tatu ya mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF III) kinatekelezwa katika Halmashauri zote 184 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar ambacho kitafikia kaya milioni moja laki nne na nusu zenye jumla ya watu milioni 7 kote nchini.
Aidha kipindi hiki cha Pili kitahakikisha kwamba huduma za jamii zinaongezwa na kuboreshwa ili kutoa huduma na kuendeleza rasilimali watoto hususan katika upatikanaji wa elimu na afya.
|
PICHANI NI DC MUHEZA NA WASHIRIKI WA MAFUNZO |
|
|
|
WASHIRIKI WA MAFUNZO |
|
|
||||
|
|
||||
|
|
|
|||
|
Mkuu wa Wilaya Mhe Halima Bulembo (aliye vaa fulana ya bluu) akiwakatika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo. |
|
|
|
Sehemu ya wataalam walioshiriki mafunzo ya mpango wa kunusuru kaya maskini yaliyofanyika kwenye ukumbi wa TATE PLUS tarehe 6/7/2021. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.