Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Halima Abdallah Bulembo amezindua wiki ya unyonyeshaji leo tarehe 6/8/2021 katika kituo cha afya Mkuzi kilichopo katika kijiji cha Mkuzi Kata ya Mkuzi ili kuongeza uelewa na kulinda afya ya mama na mtoto katika jamii.
Akizungumza katika Maadhimisho hayo Mkuu huyo wa Wilaya amesema Maziwa ya Mama yana virutubisho vyote hivyo basi watoto wanyonyeshwe miezi sita mfululizo ili kuwakinga na maradhi yanayoweza kujitokeza katika umri huo mdogo.
Aliongeza kuwa Maziwa ya mama yana umuhimu sana katika kwa mtoto kwa kuwa akinyonyeshwa vizuri kwa wakati muafaka afya yake itaimarika na kumfanya mtoto awe na uelewa wa haraka na utambuzi wa masuala mbalimbali katika maisha yake.
“Tunapokuwa na watoto wadogo tusiendekeze majukumu ya kazi zetu binafsi tukamsahau mtoto, watoto wadogo ndio jukumu letu la kwanza kwani wakikosa maziwa ya mama afya zao zitashindwa kurekebishwa katika maisha yao yote” alisema Mhe Bulembo.
Awali akisoma Risala ya siku ya Uzinduzi wa maadhimishni ya wiki ya unyonyeshaji Afisa Lishe wilaya ya Muheza Emmanuela Lawrence amezitaja faida za unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni humpatia mtoto virutubishi vyote anavyohitaji kwa uwiano sahihi wa ukuaji na maendeleo yake, hupatia kinga ya maradhi mbalimbali kama kuharisha na magonjwa ya mfumo wa hewa, husaidia tumbo la mama la uzazikurudi katika hali yake ya kawaida, huzuia upungufu wa damu, huzuia upatikaji wa mimba, huzuia saratani ya mfuko wa uzazi nay a matiti, hujenga uhusiano mzuri wa karibu kati ya mamana mtoto,
Aliendelea kuwa Maziwa ya mama ni safi na salama, hupatikana muda wote, katika joto sahihi na hayahitaji matayarisho, hayaharibiki yakiwa ndani ya matiti , hukaa saa 8 bila kuharibika katika joto la kawaida na saa 72 kwenye jokofu, huokoa muda wa mama na fedha za familia , hayaleti matatizo ya mzio, hutunza mazingira kwani hayaachi mabaki kama makopo au chupa.
Kwa upande wake mama mwenye mtoto wa miezi 5 mkazi wa kijiji cha mkuzi ambaye ni shuhuda wa kunyonyesha mtoto miezi 6 mfululizo amesema kumpatia mtoto chakula cha ziada mapema kutamletea madhara ya kupata tumbo kubwa litakalomfanya aonekane kuwa kama mwenye kwashakoo.
Afisa lishe Wilaya ya Muheza Emmanuela Lawrence(kushoto) akisoma risala kwa Mkuu wa Wilaya Muheza ambaye pia ni mgeni rasmi wa hafla | Afisa lishe Wilaya muheza Emmanuela Lawrence (kushoto) akikabidhi risala kwa Mkuu Mgeni rasmi Mhe Halima Abdallah BULEMBO | sehemu ya watumishi na wananchi walioshiriki | Sehemu ya wakina mama wanaonyonyesha |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.