Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Halima Bulembo na familia yake wamehesabiwa nyumbani kwao Mbaramo Wilayani Muheza mapema tarehe 23/8/2022 ikiwa ni utekelezaji wa wajibu wa Serikali unaomtaka kila mwananchi kuhesabiwa katika Sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022.
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi ambao hawajahesabiwa kuwa wavumilivu kwa makarani hao wa sense pindi watakapokuwa wamefika nyumbani kwao kwa kuwapa ushirikiano na kutoa taarifa za wanakaya kwa usahihi na kuhakikisha wanaandaa vitambulisho vinavyohitajika mapema.
“Tujitahidi kusikiliza kwa makini maswali tunayoulizwa na kuhakikisha tunajibu kwa ufasaha na usahihi ili kuweza kuisaidia Serikali yetu kapanga mipango ya maendeleo" alisema Bulembo.
TUJITOKEZE KUHESABIWA KWA MAENDELEO YA TAIFA |
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.