Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mh.Halima Bulembo amepiga marufuku na kukemea kitendo cha kuwapa watoto wa shule mimba au kuwa na mahusiano nao kwaatakaye bainika atapata adhabu ya kifungo cha miaka thelathini jela, kwani ameanzisha kampeni ambayo inawatafuta mabinti wote waliacha masomo kutokana na kupata ujauzito hivyo kuweza kuwasaidia kurudi mashuleni.
Bulembo ameyasema hayo jana akiwa katika ziara yakutembelea vijiji vilivyopo ndani ya kata ya Nkumba, akiongozana na baadhi ya wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya Muheza, na viongozi wengine ndani ya kata hiyo kwa lengo la kuwafahamu wananchi wa kata ya Nkumba na kusikiliza kero zao ili kuweza kuzitatuliwa.
Akizungumza na wananchi Bulembo amepiga marufuku maswala ya unyanyasaji kwa wanawake ikiwemo kitendo cha kuwapiga, na kukemia mila potofu ikiwemo Kuzuza, jambo ambalo limepelekea kuvunja amani, kwani amekuwa akipokea kesi za mauaji kutokana na suala hilo na kuwataka wananchi kuliacha mara moja, lakini pia amewataka wananchi kuacha dhana potofu juu ya suala la Sensa ya watu na makazi kwani nikwaajili ya kuboresha huduma mbalimbali za jamii.
Akiendelea kujibu kero mbalimbali za wananchi ikiwemo maswala ya umeme,afya,elimu na maji ambayo mengine yalikuwa yakijibiwa na wataalam wa sekta hizo, Bulemba amewakumbusha wanainchi wake kuendelea kuchukuwa tahadhari juu ya wimbi la tatu la Corona ikiwa ni pamoja na kupata chanjo ambayo kwa sasa inapatikana katika hospitali zote.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mh.Halima Bulembo akizungumza na wananchi wa kata ya Nkumba ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero zao na kuweza kuzitatua. | Sehemu ya wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza na viongozi mbalimbali wa kata ya Nkumba | Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kusikiliza kero |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.