Waziri wa Maji Professa Makame Mbarawa amewataka Wananchi kuwa wavumililvu katika kipindi hiki cha Ugonjwa wa Corona(COVID-19) kwani Mkandarasi ambaye ni mkazi wa Afrika kusini kwasasa hawezi kusafiri kutokana na kufungwa kwa usafiri wa anga ikiwa ni katika kuchukua tahadhari ya ugojwa wa Corona.
Aliyasema hayo alipokuwa akifanya Ziara yake Wilayani Muheza tarehe 4/4/2020 wakati akitembelea Miradi ya Maji Kilapula (PONGWE-MUHEZA) uliopo Kata ya Mlingano na Mradi wa maji Umba uliopo kata ya Ngomeni.
Aidha prof. Mbarawa amefafanua kuwa, endapo ugonjwa huu utaendelea kuchukua muda mrefu Serikali itachukua hatua ya kutatua tatizo hili ili Wananchi waweze kupata Maji kwa wakati kwa sababu Maji ni muhimu kwa matumizi ya binadamu kiafya.
Lakin pia, alipokuwa katika Mradi wa Maji PONGWE-MUHEZA Prof. Mbarawa amemtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya KORERG Steven Lucas kuukamilisha kwa kufunga Pampu na kusambaza maji kwa haraka ili Wananchi waweze kuondokana na adha ya Maji kwa kipindi hiki cha mlipuko wa Corona (COVID-19).
Mbali na hilo, Prof. Mbarawa ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Milioni 150 kwa ajili ya kuanza upya ujenzi wa Mradi wa maji Kilongo, kuchimba Mitaro na ununuzi wa Mabomba.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri wa Wilaya ya Muheza ambaye ni Diwani wa kata ya Ngomeni Bakari Mhando ametoa ombi kwa Waziri wa maji kama tazizo kubwa nikufungwa kwa pampu suala hili lifanyiwe kazi maana ndoo ya moja ni shilingi elfu moja na ukizingatia kwa sasa kuna ugonjwa wa Corona hiyo ni changamoto.
“Natoa maelekezo Wizara ya Maji changamoto kubwa ni kwa upande wa Manunuzi Pesa inatolewa kwa muda husika wao wanachelewesha kuifanyia kazi na kama wataendelea kufanya hivyo tutawachukulia hatua Watendaji hao”.amesema Mbarawa.
Mhandisi wa Maji Halmashauri Wilaya ya Muheza Cleophace Maharangata akizungumza walipotembelea Mradi wa Maji Umba tarehe 04/04/2020. | Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Mwanasha Rajab Tumbo akitoa shukrani kwa Waziri wa Maji kwa kutembelea Mradi wa Maji Umba. | Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ambaye ni Diwani Kata ya Ngomeni Mhe. Mhando (wapili kutoka kulia) akizungumza walipotembela katika Mradi wa maji Umba. |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.