Chanjo ya ugonjwa wa corona (uviko -19) imetolewa jana tarehe 4/8/2021 katika kituo cha afya ubwari kilichopo katika kitongoji cha Mbaramo kata ya MBARAMO Wilayani Muheza ili kujikinga na huo hatari unaoenezwa kwa njia ya kugusa majimaji yatokayo puani na mdomoni.
Uzinduzi wa chanjo hii ulifanywa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Halima Abdallah Bulembo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo;
Uzinduzi huo ulishirikisha kamati ya ulinzi na usalama wilaya Muheza, watumishi wa Halmashauri na wananchi wote wa Wilaya hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Halima Abdallah Bulembo amewataka watumishi na wananchi wajitokeze kwa wingi kupata chanjo hiyo ili waweze kujikinga na ugonjwa huo na kuwahakikishia kuwa chanjo hiyo ni salama
DC AKIPATIWA CHANJO YA UVIKO-19 | KATIBU TAWALA AKIPATA CHANJO | AFISA UTUMISHI MUHEZA AKIPATA CHANJO | MGANGA MKUU MUHEZA AKIPATA CHANJO | SEHEMU YA WATUMISHI NA WANANCHI WALIOSHIRIKI |
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Abdallah Bulembo akipata chanjo ya corona leo jana tarehe 4/8/2021 katika kituo cha afya ubwari kilichopo katika kata ya Mbaramo. | Katibu Tawala Wilaya Muheza Bi Desderia Haule akipata chanjo ya Uviko wa 19 jana tarehe 4/8/2021 katika kituo cha afya Ubwari ili kujikinga na Maambukizi ya corona | Afisa Utumishi Wilaya ya Muheza Bw. Godhelp Ringo akipata CHANJO ya corona katika kituo cha Afya ubwari jana tarehe 4/8/2021 ili kujikinga na ugonjwa wa uviko - 19 | Mganga Mkuu Wilaya ya Muheza Dkt Flora Kessy akipata chanjo ya corona katika kituo cha afya ubwari ili kujikinga dhidi ya virusi vya Corona | Sehemu ya Watimishi na wataalam walioshiriki katika zoezi la utoaji chanjo jana tarehe 4/8/2021 katika kituo cha afya ubwari. |
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.