Bomba la mafuta ambalo linatarajiwa kupita katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya muheza ikihusisha kata ya Lusanga, Muheza, Bwembwera, Kwakifua,Kilulu,Ngomeni, na Mlingano hivyo serikali kuomba wananchi wa Muheza kujitokeza kwenye fursa mbalimbali wakati wa ujenzi wa bomba hilo.
Katika mradi huo serikali imetoa huduma 12 kwa wananchi wake ikiwemo vifaa vya ujenzi,vyakula,usafirishaji,mitambo ya kupakuwa mizigo,kandarasi za ujenzi,utunzaji wa mazingira mbali na hayo fursa mbalimbali za ajira ikiwemo vibarua,madereva,wahasibu,wafanya usafi,maforodha,watunza stoo,wachomeleaji,waendesha mitambo, na huduma nyingine mbalimbali za kijamii ili kuwezesha utekelezaji mzima wa ujenzi wa bomba hilo.
Aidha ujenzi wa bomba la mafuta ni mradi wenye jumla ya kilometa 1,443 kutoka magharibi mwa Uganda mpaka kwenye bandari ya hindi Tanga, ambapo katka mkoa wa Tanga mradi utapita katika wilaya ya Tanga yenyewe, Muheza, Kilindi, Handeni.
Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa maendeleo Wilaya ya Muheza Bi. Vije Mfaume Mbwanga akizungumza na wafanyabiashara wa Muheza jana katika kikao kilichokuwa kinahusu fursa mbalimbali zitakazojitokeza katika ujenzi wa bomba la mafuta. | Mratibu wa mradi wa bomba la mafuta Bw. Asidi Mrutu akiongea na wafanyabiashara wa Muheza. | Baadhi ya wafanyabiashara wa Muheza waliohudhuria kikao cha bomba la mafuta. |
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.