Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga limepitisha Mapendekezo ya Makisio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Jumla ya Bilioni 47 kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Awali akiwasilisha Umbile la Mapendekezo ya Makisio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ya Kiasi cha Bilioni 47,262,554,292. Afisa Mipango Wilaya ya Muheza Daniel Mwakitalu amesema Fedha hizo kwa ajili ya Mishahara ni Bilioni 32,479,952,000, Miradi ya Maendeleo Bilioni 10,310,987,149 na Matumizi mengineyo Bilioni 1,290,905,000 ambapo Bajeti imezingatia Mpango wa Maendeleo endelevu wa Mwaka 2030, sambamba na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Cyprian Mselemu alipokuwa akifunga Baraza hilo ametoa Wito kwa Wtumishi kutunza Siri za Serikali na Sio kutumia Mitandao mbalimbali ya kijamii katika kusambaza taarifa za siri za Serikali badala yake watumie Mitandao hiyo uleta katika kuleta Maendeleom ya Wilaya ya Muheza.
Amesema baadhi ya watumishi wa Serikali wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kutoa siri za za Serikali hivyo amewaomba kutumia mitandao hiyo kwa ajili ya kuisaidia Serikali na kujiletea Maendeleo.
“Ni waombe watumishi wenzangu tuwe makini na matumizi ya Mitandao ya kijamii, tusiiitumie kutoa siri za Serikali badala yake tutumie mitandao hiyo ya kijamii kuisemeaa vizuri Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri inyofanywa ya kuiletea maendeleo Wilaya ya Muheza” alisema Mselemu.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Tanga Lazaro Saulo amepongeza Halmashauri ya Muheza kwa Juhudi za Idara ya Utumishi kwa hatua za kuhakikisha wanangalia M,aslahi ya Watumishi kwa Ukaribu sana ikiwemo Upandishaji wa Madaraja na Malipo mbalimbali ambayo walikuwa wakilalamikia.
“Amesema Watumishi wa kada zote wamekuwa na Maumivu ya muda mrefu juu ya maswala ya Madeni, kupanda Madaraja hivyo kama Serikali kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Utumishi na Afisa Utumishi mmefanikiwa kuanza kumaliza kilio hicho kuongeza hali ya watumishi kufanya kazi kwa bidii pia ameshauri idara ya Utumishi kuzingatia upandishji wa madaraja kwa watumishi wote ili kuepuka Msemo wa tumekusahau wakati tunapitisha wafanyakazi ambao wanapaswa kupandishwa.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.