Kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika April 30, 2020 katika ukumbi wa TATE PLUS uliopo katika kata ya Genge kimeazimia Wananchi wote wanapotoka majumbani na wanapokuwa katika maeneo yao ya kazi wavae barakoa ikiwa ni tahadhari ya ugonjwa wa Corona.
Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ambae ni Mwenyekiti wa kikao cha baraza la Madiwani na Diwani kata ya Ngomeni Mhe, Bakari Zuberi Mhando amesema kwa kuwa hali ya Maambukizi inaongezeka kila siku hapa nchini ni vyema kila Mwananchi anapotoka nje ya nyumba yake avae barakoa ili kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona.
Pia alimtaka Mmiliki wa Vyombo vya Muziki SADICK mwenye tabia ya kupiga Muziki usiku maeneo ya njia ya kwenda Magila aache tabia hiyo mara moja kwani itasababisha mkusanyiko na kupelekea kuleta Maambukizi Wilayani.
Nae Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Mhandisi Mwanasha Rajab Tumbo amewataka wanachi kuacha tabia ya Mkusanyiko msibani wanaotakiwa kuhudhuria kwenye tukio hilo ni watu wasiozidi kumi (10) tu ili kuepuka msongamano katika eneo husika.
Pia aliwataka Waheshimiwa Madiwani wakatoe elimu katika maeneo yao kwani suala la ugonjwa wa Corona linahitaji elimu ya kutosha kwa wananchi, pia aliwataka watoe msaada wa michango ya vifaa tiba au fedha ili kuweza kufanikisha kutokomeza janga hili.
“Twendeni Waheshimiwa tukatoe elimu kwa wananchi wetu , tunao wajibu sisi kama viongozi kutekeleza jukumu hili” alisema Mkuu wa Wilaya Muheza.
Akijibu swali aliloulizwa ni kwa namna gani Halmashauri inasaidia katika kupambana na Ugonjwa huu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Nassib MMbagga amesema Halmashauri inasaidia kununua vifaa tiba na kinga kwa ajili ya wataalam waliopo katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Akieleze kuhusu kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaokuwa wameshindwa kuvaa barakoa na kuchukua tahadhari nyingine juu ya ugonjwa wa Corona Mkurugenzi Mtendaji Wilaya amesema kwa atakaeshindwa kuweka Ndoo ya Maji na Sabuni nyumbani na katika eneo la biashara yake baada ya elimu inayotolewa na wataalam huko majumbani faini itakuwa ni TZS 50,000/ (Elfu hamsini) pia amelitaka baraza kuweka sheria ya pamoja ya kusimamia agizo hili.
“Tuacheni tuendelee kutoa elimu kwa wananchi, wale wajeuri watakaoshindwa kutekeleza maelekezo tutahangaika nao, nitachukua hatua, nikiwachukulia hatua mnyamaze” alisema Mkurugenzi MMBAGGA.
Akifafanua namna ya uvaaji wa barakoa Mganga Mkuu Wilaya amesema Barakoa moja huvaliwa kila baada ya Masaa 4-6 hivyo basi kila mmoja anatakiwa kutembea na barakoa zaidi ya mbili mfukoni mwake, aliongeza kuwa mtu anapovaa barakoa hatakiwi kujishikashika usoni kwani anaweza kujisababishia maambukizi.
Aidha alijibu swali la ushonaji wa barakoa za vitambaa kuwa barakoa ya kitambaa inatakiwa kuwa na’ layer’ tatu ambapo layer ya katikati inatakiwa kuwa na stiff ili kusaidia hewa kupita kwa urahisi na material ya kitambaa kinachotakiwa ni Cotton.
Aliongeza kuwa barakoa ya kitambaa ikivuliwa ihifadhiwe vizuri kwenye mfuko ukifika nyumbani ifuliwe kwa sabuni nyingi na kunyooshwa kabla haijavaliwa tena wakati barakoa za madukani (disposable) zikivuliwa zichomwe moto.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Nassib Mmbagga akisisitiza Uvaaji wa barakoa wakati wa kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika April 30, 2020 katika ukumbi wa Tate Plus. | Diwani kata ya Genge Mhe, Mtiga Adam Lubawa akizungumza wakati wa Kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika April 30, 2020 katika Ukumbi wa Tate Plus |
|
|
|
BAADHI YA WATAALAM WAKIZUNGUMZA WAKATI WA BARAZA
DMO Flora kessy. Meneja TARURA kahoza
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.