Baraza la Madiwani la Halmashauriya Wilaya ya Muheza limepitisha bajeti ya Shilingi bilioni 41.2 ambayo itatekelezwa katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2022/2023.
Akiwasilisha bajeti hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Nassib Mmbagga amesema kuwa kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 9.67 ni fedha za Miradi ya Maendeleo ikiwa Shilingi Bilioni 28.09 ni ruzuku ya Malipo ya Mishahara hivyo basi Ruzuku ya Matumizi kutoka Serikali kuu ni Shilingi Bilioni 38.70.
Aidha Mkurugenzi Nassib Mmbagga amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imejipanga kukusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 2.54 kutoka kwenye Mapato yake ya ndani ambazo ni sawa na ongezeko la Shilingi Bilioni 4.67 la bajeti inayoishia Mwaka huu wa fedha 2021/2022.
Mmbagga aliendelea kufafanua kuwa Halmashauri inatarajia kupokea Shilingi Bilioni 38.70 ambayo ni Ruzuku ya Malipo ya Mishahara kutoka Serikali kuu ikiwa kiasi hicho ni sawa na ongezeko la Shilingi Bilioni 15.6 ukilinganisha na bajeti ya Mishahara inayaoishia Mwaka huu wa fedha 2021/2022 ambayo ni Shilingi Bilioni 23.04.
Akielezea utekelezaji wa Makusanyo amesema mpaka sasa Halmashauri imefikia asilimia 61 ya makusanyo katika vyanzo vyake vya mapato ya ndani.
Awali akisoma mapendekezo ya mpango na bajeti wa Halamshauri kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 afisa Mipango wa Wilaya hiyo Pascal Temba amesema katika kipindi cha Mwezi Julai hadi Disemba 2021 Halmashauri ya Muheza ilikisia kupokea Ruzuku, na Makusanyo ya Mapato yake ya ndani Shilingi Bilioni 36.57 ambapo hadi kufikia disemba 2021 kiasi cha shilingi Blioni 17.40 kilikusanywa ambayo ni sawa na asilimia 48 ya Makusanyo.
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.