Afisa Maendeleo ya Jamii wamefanya ziara ya wanafunzi wa Msingi na Sekondar katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kutoa Elimu ya kupinga Ukatili kwa Watoto chini ya umri wa miaka 18.
Elimu hiyo imetolewa siku mbili 21 na22/1/2025 katika jumla ya Shule 13, Msingi 8 na Sekondari 5 yenye lengo la kupunguza matukio ya Ukatili wa kijinsia na kuimarisha au kuchochea hali ya kujitambua kwa Watoto na Wanafunzi,kuimarisha hali ya ulinzi na hivyo kuweza kufikia malengo yao kitaaluma.
Wakati wa ziara hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Bi Husna Herry amewaasa Wanafunzi kutoa Taarifa bila kusita ya vitendo vya ukatili bila kufumbia macho na amewasisitiza kuwa wana Haki na Wajibu kama wanafunzi na Watoto
Nae Afisa Maendeleo Bw Selemani Mngodo amewaasa wazai kuwajibika kwenye majukumu ya Msingi ikiwemo suala la malezi na makuzi ya Watoto. Pia amewashauri Walimu kuendelea kuimarish ulinzi wa Watoto kupitia Mradi wa Shule Salama na kuweka vibao mashuleni vyenye jumbe mbalimbali za kupinga Ukatili kwa Watoto
Idara ya Maendeleo kwa jamii imefanikiwa kuwafikia Wanafunzi 5413, Wakike 2825, Wakiume 2588, Wanafunzi 1372 ni wa Sekondari ikiwa Wakike ni 791 Wakiume 585, Shule za msingi jumla ni Wanafunzi 4037 walitembelewa Wakiume 2003, Wakike 2034
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.