Mbunge wa Jimbo la Muheza Mhe balozi Adadi Rajabu afanya kikao na Wadau wa Jukwaa la Machungwa leo katika ukumbi wa mikutano wa Chama Cha Walimu(CWT) baada ya kuona machungwa yanakosa soko wilayani humo.
Akizungumza katika kikao hicho Adadi amesema ili kuweza kupata soko zuri la machungwa ni lazima kuwe na mshikamano wa pamoja utakaowawezesha wakulima wa machungwa kusimama imara katika biashara yao hali itakayopelekea kuwa na bei elekekezi, aidha amewataka wakulima kuunda vikundi ili waweze kukopesheka kwenye taasisi za kifedha kama benki.
Aliongeza kuwa uwepo wa umoja husaidia kuleta msimamo katika biashara zao hali itakayopelekea kuuza machungwa kwa gharama yoyote watakayo ili waweze kuleta maendeleo katika kaya zao , Pia aliwazitaka Taasisi za mikopo kuwa na masharti nafuu ili kuwafanya wakulima waweze kukopa .
Akitoa ufafanuzi wa taratibu za upatikanajia wa mikopo kwa wakulima Kaimu Meneja wa Benki ya NMB BI Neema Maro amesema kuna kitengo kijulikanacho kama NMB foundation ambacho hutoa elimu kwa mkulima wa chungwa ili aweze kuvuna chungwa bora na kuwatafutia soko wakulima wa zao hilo ndani na nje ya nchi. Aliongeza kuwa ili mkulima apewe mkopo antakiwa awe amesajiliwa na kufungua akaunti ya NMB, Riba ya mkpo huo ni asilimia 17.
Nae mratibu wa wadau wa kilimo Tanzania Bi. Asha Mbelwa ameshauri wadau wa machungwa wakawatembelee wakulima na kuwaelimisha kuhusu madalali ambao mara nyingi ndio wanufaika wa biashara ya zao la chungwa kuwa wanavuruga biashara ya mkulima kwa kujipatia fedha nyingi na kumuacha mkulima akiwa masikini.
Kwa upande mwingine Diwani wa kata Nkumba mhe, Charles Mhilu ameshauri kuwepo kwa mfumo wa urasimishaji wa wakulima na madalali kiwilaya na Mkoa ili kupiga marufuku uuzaji wa machungwa holela kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi.
“ili tufanikiwe lazima tutengeneze lazima tutengeneze mfumo wa Mkoa na Wilaya wa kuwathibitisha wakulima kufanya biashara ipasvyo ili kupiga marufuku uuzaji kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi” alisema Mhilu.
Wakitoa maazimio ya kikao hicho kilichoketi mnamo tarehe 21\2\2019 wadau wa jukwaa la wauza machungwa wamesema ni marufuku mtu yeyote kupepea machungwa na atakaekamtwa atatozwa faini ya kuanzia elfu 50 na mazao yake yatateketezwa, wakulima wasiwekeze mazao byao bali wakakope kwenye vyombo vya kifedha, wakulima wabuni vyanzo vingine vya mapato sio kuwekeza mazao , viongozi wasimamie sheria ndogo za mazao ipasavyo.
|
|
|
---|---|---|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|||||||||
|
|
|
|||||||||
|
|
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.