1.Kila mwananchi anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa analazimika kulipa kodi ya ardhi kwa kila mwaka.
2.Kila mmiliki wa kiwanja au shamba lililopimwa analazimika kwenda Ofisi ya Ardhi Wilaya akiwa na Stakabadhi ya Malipo ya Kodi ya Ardhi kwa mwaka uliopita pamoja na Hati Halisi ya Umiliki wa kiwanja au shamba hilo.
3.Mtaalamu wa Mfumo wa Kodi ya Ardhi atamtolea Hesabu ya Malipo anayotakiwa kulipa kwa mwaka husika au malimbikizo ya deni la Kodi ya Ardhi ikiwa ni pamoja na faini.
4.Malipo yanaweza kufanyika kwa njia ya simu kwa kufuata maelekezo kwa kubofya namba hizi * 152*00# kisha endelea kufuata maelekezo.
5.Mara baada ya kiwanja kupimwa unatakiwa kulipia hati ndani ya siku 90.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.