UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA
Leseni zinazotelewa na Halmashauri za Wilaya, Manispaa, Miji na Majiji ni za Kundi B. Leseni za Kundi A hutolewa na Wizara ya Viwanda na Biashara
Mfano wa Biashara zilizo kwenye Kundi B:
Wakala wa Bima (Insurance Agent)
Vipuri (Spare parts, Mashine tools)
Maduka ya dawa za Binadamu/Mifugo
Viwanda Vidogo (Small Scale Manufacturely and Selling)
Uuzaji Bidhaa Jumla na Rejareja (Wholesale and Retail trade) n.k
Baadhi ya Masharti/Nyaraka zinazohitajika kama kiambatanisho na masharti katika maombi ni ;
Masharti mengine ya kupata leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha e.g. Mgahawa, Dawa za Binadamu na Mifugo, Vyakula,Nyama na Samaki inabidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake
Hati ya Utaalam (Professional Certificates) kwa biashara zote za kitaalam mfano ushauri wa kitaalam ( consultancy, uhandisi)
Hati ya kiuwakilishi (powers of attoney ) Iwapo wenye hisa wote wa kampuni wapo nje ya nchi itolewe kwa Mtanzania anaeishi hapa.
Ushahidi wa Maandishi kuwa ana mahali pa kufanyia biashara ( kwa mfano hati ya za nyumba, mkataba wa upangishaji, risiti za malipo ya kodi za majengo aua ardhi.
kwa leseni zinazothibitishwa na Mamlaka mbalimbali kama vile TFDA, EWURA, TCRA,CRB, TALA, CAL lazima kwa na leseni ya biahara husika kabla ya kuomba leseni ya biashara
Maombi mapya yatapitia ngazi za Serikali ya Mtaa/kijiji, Afya na Kisha Ofisi ya Biashara kwa ajili ya utoaji wa leseni.
ANGALIZO: Leseni za biashara hulipwa ada na kuhuishwa (renew) kila mwaka kwa mujibu wa sheria ya leseni za biashara No 25ya mwaka 1972 na mabadiliko yake ya mwaka 2014 na 2015.
Pakua Fomu ya Maombi ya Leseni ya Biashara.pdf
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.