1. Kulipa gharama za kuandaliwa hati miliki ambazo ni Primiamu, Ada ya Maombi ya Kiwanja, Ada ya Soroveya, Gharama ya Malipo ya Ramani kwa Ajili ya Kuandaliwa Hati, Malipo ya Hati, Malipo ya Stampu, Malipo ya Kodi ya Ardhi na Malipo ya Usajili wa Kiwanja husika.
2. Baada ya kukamilika kwa malipo hayo yote, atatakiwa kuwasilisha Kitambulisho chochote kinachokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi kama vile Nida, Mpiga Kura, Cheti cha Kuzaliwa n.k.
3. Atatakiwa pia awasilishe Picha Sita za Pasipoti Saizi za Rangi za hivi karibuni.
1. Halmashauri kujenga hoja juu kuhusu uwepo wa haja ya kuandaa mpango wa urasimishaji.
2. Halmashauri kupitisha azimio lakuandaa mpango wa urasimishaji.
3. Halmashauri kutoa tangazo kwenye gazeti la serikali na magazeti yanayosomwa katika eneo linalokusudiwa kuandaliwa mpango wa urasimishaji na kuweka matangazo kwenye mbao za matangazo katika eneo husika.
4. Kuitisha mkutano wa wadau wote katika eneo litakaloandaliwa mpango wa urasimishaji.
5. Mkutano wa wadau utakaokuwa na matokeo chanya halmashauri itasaini makubaliano na kuunda Kamati ya urasimishaji.
6. Kamati ya urasimishaji itaandaa inventory ya nyumba, huduma, ubora wa ardhi, taratibu za umiliki matumizi ya ardhi yaliyopo na miundombinu iliyopo katika eneo husika kama vile umeme, maji n.k.
7. Kukubaliana taratibu za uandaaji wa mpango wa urasimishaji katika eneo husika kama vile;
(a)Kulipia gharama za mchoro wa mipango miji na gharama za soroveya.
(b)Kulipia gharama za za mchoro wa mipango miji na soroveya kuwasilishwa Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kupitishwa.
(c)Kulipa gharama za kuandaliwa hati miliki ambazo ni Primiamu, Ada ya Maombi ya Kiwanja, Ada ya Soroveya, Gharama ya Malipo ya Ramani kwa Ajili ya Kuandaliwa Hati, Malipo ya Hati, Malipo ya Stampu, Malipo ya Kodi ya Ardhi na Malipo ya Usajili wa Kiwanja husika.
(d)Baada ya kukamilika kwa malipo hayo yote, atatakiwa kuwasilisha Kitambulisho chochote kinachokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi kama vile Nida, Mpiga Kura, Cheti cha Kuzaliwa n.k..
(e)Atatakiwa pia awasilishe Picha Sita za Pasipoti Saizi za Rangi za hivi karibuni.
1. Kuwasilisha ombi la kutaka kupimiwa ardhi ya shamba lake kwa Halmashauri ya Kijiji husika.
2. Kujadiliwa ombi lake la kutaka kupima shamba lake na Halmashauri ya Kijiji husika.
3. Halmashauri ya Kijiji husika wataandika muhtasari iwapo watakuwa wamekubali ombi hilo.
4. Halmashauri ya Kijiji husika itaitisha Mkutano Mkuu wa Wanakijiji wote ili kujadili ombi hilo la kutaka kuhawilisha ardhi hiyo.
5. Wanakijiji wakiridhia ombi hilo la kuhawilisha ardhi, Mwenye Shamba ataandika barua yenye kuambatana na mihtsari yote miwili kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, kuomba kuhawilisha shamba lake.
6. Mkurugenzi Mtendaji Wilaya akiridhia, Mwenye Shamba atatakiwa kuhakikisha kuwa Afisa Ardhi Mteule Wilaya na Mkuu wa Wilaya wanafika katika kijiji husika na kufanya Mkutano Mkuu wa Hadhara wa Wanakijiji wote ili kujiridhisha na maombi haayo ya kuhawilisha ardhi.
7. Wanakijiji wakiridhia uhawilishaji huo wa ardhi mbele ya Mkuu wa Wilaya na Afisa Ardhi Mteule Wilaya, Afisa Ardhi Mteule ataandika barua kwenda kwa Waziri wa Ardhi ili kumtaarifu kuhusu ombi hilo la uhawalishaji wa ardhi.
8. Waziri wa Ardhi akikubali uhawilishaji huo wa ardhi, Mwenye Shamba ataandika tangazo la kusudio la kuhawilisha ardhi hiyo na kuliweka kwenye shamba husika kwa muda wa siku 90.
9. Kama hakuna pingamizi lolote litakalotolewa na mtu yeyote, taratibu za kuhawailisha shamba hilo zitaendelea kwa mujibu wa sheria za ardhi.
10. Atatakiwa kulipia gharama za mchoro wa mipango miji na gharama za soroveya.
11. Atatakiwa kulipia gharamza za mchoro wa mipango miji na soroveya kuwasilishwa Wizara ya Ardhi kwa ajili ya kupitishwa.
12. Atatakiwa kulipa gharama za kuandaliwa hati miliki ambazo ni Primiamu, Ada ya Maombi ya Kiwanja, Ada ya Soroveya, Gharama ya Malipo ya Ramani kwa Ajili ya Kuandaliwa Hati, Malipo ya Hati, Malipo ya Stampu, Malipo ya Kodi ya Ardhi na Malipo ya Usajili wa Kiwanja husika.
13. Baada ya kukamilika kwa malipo hayo yote, atatakiwa kuwasilisha Kitambulisho chochote kinachokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi kama vile Nida, Mpiga Kura, Cheti cha Kuzaliwa n.k.
14. Atatakiwa pia awasilishe Picha Sita za Pasipoti Saizi za Rangi za hivi karibuni.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.