Tuesday 3rd, December 2024
@MAJENGO SHIMONI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan kesho tarehe 16/3/2021 saa 2:00 asubuhi atawasili katika eneo la majengo shimoni akitokea wilayani KOROGWE
Katika Ziara yake atapata fursa ya kutembelea miradi miwili (2) ya maendeleo ambayo ni Mradi Hospitali ya Wilaya ya Muheza uliopo katika kijiji cha Tanganyika kata ya Lusanga na Mradi wa Maji PONGWE- MUHEZA uliopo katika kijiji cha Muungano kata ya Mlingano.
Katika hatua nyingine ataweka jiwe la msingi katika miradi hiyo ya maji na mradi wa Hospitali ya Wilaya Muheza.
Aidha atasalimiana na wananchi wa wilaya ya Muheza katika eneo la majengo Shimoni lililopo katika kitongoji cha majengo kata ya majengo .
Shime Mwananchi njoo majengo shimoni umlaki, na kumsikiliza mama Samia Suluhu Hassani Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.