Thursday 21st, November 2024
@MUHEZA
Katika semina ya waandikishaji wapiga kula iliyofanyika katika ukumbi wa CWT Muheza msimamizi wa uchaguzi Pascal Temba amewaomba waandikishaji wapiga kula kufungua vituo kwa wakati kuanzia saa 02:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni amesisitiza kwa kuwaomba kufungua vituo kwa siku zote saba. Mafunzo hayo yaliambatana na kuelimishwa majukumu yao katika kuandikisha wapiga kura.
“Kabla hujampatia mpiga kura karatasi za kupigia kura, hakikisha umejiridhisha kama jina la mpiga kura limeorodheshwa katika orodha ya wapiga kura na baada ya kujiridhisha utatakiwa kuomba mpiga kura ajitambulishe kwa kutumia kitambulisho kimoja kati ya vitambulisho vifuatavyo kitambulisho cha mpiga kura, kitambulisho cha kazi,, hati ya kusafiria, kadi ya bima ya afya, kitambulisho cha shule au chuo, kitambulisho cha mifuko ya hifadhi ya jamii, leseni ya udereva au kitambulisho cha taifa”, alisema msimamizi wa uchaguzi Pascal Temba katika semina ya waandikishaji wapiga kura.
Baada ya semina kuisha wasimamizi wa vituo walipata nafasi ya kuapa kwa ajili ya kuanza kazi rasmi ya uandikishaji wapiga kura. Semina iliambatana na ugawaji wa mabango ya kubandika katika vituo vya kupigia kura. Amewaomba kubandika mabango hayo kwa wakati ili wananchi waweze kuona vituo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.