Tuesday 3rd, December 2024
@KITUO CHA AFYA UBWARI
“KILA TONE LA CHANJO YA POLIO LITAIWEKA TANZANIA SALAMA DHIDI YA UGONJWA WA KUPOOZA”
Uzinduzi wa chanjo ya ugonjwa wa polio utafanyika kesho alhamisi tarehe 19/5/2022 kuanzia saa 2:30 asubuhi katika Kituo cha afya Ubwari kilichopo katika kitongoji cha Mbaramo kata ya Mbaramo Wilayani Muheza.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni MKuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Halima Abdallah Bulembo ambaye ataongoza shughuli hiyo.
Zingatia kumpeleka mtoto mwenye umri chini ya miaka 5 yaani mwenye Mwezi 0-59 akapatiwe huduma stahiki ili umkinge dhidi ya ugonjwa wa kupooza ambao unaweza kusababi sha ulemavu wa ghafla, kudumu na hata kupoteza maisha .
Kumbuka: hata kama ameshapata chanjo hii kwenye utaratibu wa kawaida anastahili kupata chanjo tena.
“EWE MZAZI AU MLEZI HAKIKISHA MWANAO ANAPATA CHANJO HII YA MATONE ILI KUMKINGA DHIDI YA UGONJWA WA POLIO”
“Mpe matone okoa maisha”
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.