Saturday 23rd, November 2024
@MUHEZA
Kutakuwa na uzinduzi wa mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (CHF). Utakao fanyika tarehe 10/10/2019, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa wilaya Muheza. Uzinduzi huo utafanyika soko la samaki la zamani (karibu na msikiti mkubwa) kuanzia saa tisa alasiri. Uzinduzi huo utaambatana na utoaji wa elimu kwa wananchi juu ya CHF iliyoboreshwa pamoja na mada mbalimbali za afya.
Ewe mwananchi jiandikishe katika mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa (CHF) kwani gharama zake ni nafuu utalipia kwa mwaka elfu thelathini (30,000/=) tu kwa kaya ya watu sita yaan baba, mama na watoto wenye umri chini ya miaka 18, utapatiwa matibabu kuanzia ngazi ya zahanati, kituo cha afya, hospitali ya wilaya na hospitali ya mkoa kwa kufuata taratibu za rufaa.
‘WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA, JALI AFYA YAKO KWA KUWA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII ULIOBORESHWA’.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.