Friday 29th, March 2024
@TATE PLUS
Uzinduzi wa Mkutano baraza la kwanza la madiwani kwa kipindi cha Mwaka 2020/2025 utafanyika kesho jumatano tarehe 16/12/2020 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika ukumbi wa TATE PLUS uliopo katika kitongoji cha Genge kata ya GENGE Wilayani MUHEZA.
Hafla ya uzinduzi huo utakwenda sambamba na zoezi la kuwaapisha Waheshimiwa Madiwani waliopata ridhaa ya kuwaongoza na kuwatumikia wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza.
Pia kutakuwa na zoezi la kuchaguzi uongozi wa baraza la madiwani utakaosimamiwa na Katibu Tawala Wilaya Muheza Bi Desderia Haule ambapo miongoni mwa viongozi watakaochaguliwa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Muheza.
Aidha kamati nne(4) za kudumu za baraza la madiwani zitaundwa, ikiwemo kamati ya fedha uongozi na mipango, kamati ya huduma za jamii, kamati ya Uchumi ujenzi na mazingira na kamati ya kudhibiti ukimwi.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.