Thursday 21st, November 2024
@uwanja wa jitegemee
“Muheza jogging sports and club” ni klabu iliyoanzishwa Mwaka 2014 ikiwa na lengo la kufanya mazoezi ili kujiepusha na Magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, Presha ambayo yamekuwa tishio kwa afya za binadamu na mara nyingi husababisha kifo.
Klabu hii ina wanachama 156 ambao ni wakazi wa Muheza na nje ya Muheza ikiwa lengo ni kuleta mahusiano mazuri baina ya wakazi wa Muheza na maeneo ya jirani.
Muheza jogging ina kaulimbiu isemayo Mazoezi kwa afya, Mazoezi tiba, Mazoezi kwa pamoja ikiwa na maana kuwa iwapo kila mwananchi atahamasika kujiunga na klabu hiyo ataimarisha na kutibu afya yake.
Mnamo siku ya jumapili tarehe 7/8/2022 Muheza Jogging Sports and club inatarajia kufanya Bonanza la kuadhimisha Miaka nane (8) ya uanzishwaji wa klabu hiyo katika uwanja wa Jitegemee kuanzia saa 12:00 asubuhi .
Miongoni mwa shughuli zitakazofanyika kutakuwa na mashindano ya kuvuta Kamba, kushindana kula chakula, utalii wa ndani, mashindano ya Mpira wa Miguu kati wanaume waliooa na wasiooa
sanjari , kufanya jogging, kutoa elimu ya sensa ya watu na makazi na kuhamasisha watu kupata chanjo ya corona.
“Ewe mwananchi shiriki kikamilifu katika bonanza hili ili uweze kuboresha afya yako
Afya yako, uhai wako nenda kafanye Mazoezi”.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.