Thursday 21st, November 2024
@TATE PLUS
Mafunzo ya TASAF Kipindi cha Pili Awamu ya Tatu yamefanyika Muheza mnamo tarehe 16/6/2020 katika Ukumbi wa TATE PLUS uliopo katika Kitongoji cha GENGE Kata ya Genge Wilayani MUHEZA ambapo Wakuu wa Idara, na Wawezeshaji walipatiwa mafunzo hayo.
Mgeni rasmi katika Mafunzo hayo alikuwa ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa TASAF Makao Makuu Bw. PAULO KIJAZI ambae alifungua kikao na kusoma taarifa ya Utekelezaji wa Kipindi cha Kwanza cha Awamu ya Tatu ya TASAF kuwa inaonyesha kwamba Mpango wa kunusuru kaya Maskini umechangia kwa kiasi kufikiwa azma ya Serikali ya kupunguza Umaskini Nchini.
Zoezi la uhakiki wa taarifa za Walengwa utafanyika kwa njia ya simu ili kutekeleza agizo la Rais JOHN POMBE MAGUFULI kuondoa dhana iliojengeka kwa jamii ya kuwemo walengwa hewa wasiostahili wakiwemo Watu wasio maskini, Viongozi, Waliohama na Waliofariki.
Uhakiki huo utazingatia tahadhali zote za ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaosababishwa na VIRUS vya CORONA , kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kukaa umbali wa mita moja baina ya mtu na mtu, kuepuka kushikana Mikono, kunawa mikono kwa Maji tiririka na sabuni, kutumia Vitakasa mikono na kuvaa barakoa.
Aidha Kipindi cha Pili cha TASAF Awamu ya Tatu kitatekelezwa katika Halmashauri zote 185 za Tanzania Bara na Wilaya zote za Zanzibar. Utekelezaji huo utafanyika kwenye vijiji/mitaa/shehia zote nchini na kujumuisha maeneo ya vijiji/mitaa/shehia ambayo hayakupata fursa hiyo katika Kipindi cha Kwanza cha utekelezaji wake ambacho kimekamilika. Kipindi hiki cha pili kitafikia kaya 1,450,000= zenye zaidi ya watu Milioni 7 kote Nchini.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.