Thursday 21st, November 2024
@KITUO CHA AFYA
Maadhimisho ya wiki ya unyoshaji duniani hufanyika Agosti 1 ya kila Mwaka ikiwa na lengo ya kukumbushana umuhimu wa unyonyeshaji Maziwa ya mama mfululizo kwa mtoto mwenye umri wa kuanzia siku 0 hadi miezi 6 bila kupatiwa kitu kingine chochote isipokuwa maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa afya.
Kiwilaya Maadhimisho haya yatafanyi.ka siku ya ijumaa tarehe 5/8/2022 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika kituo cha Afya Ubwari.
Mgeni rasmi katika hafla hii atakuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Mhe Moses Siwa Kisiki ambaye pia ni Diwani kata ya Genge.
Kaulimbiu ya wiki ya unyonyeshaji mwaka huu 2022 inasema “ Chukua hatua, endeleza unyonyeshaji, Elimisha na toa msaada ikiwa na lengo la kuhimiza kina mama kuwanyonyesha watoto ili kukuza na kulinda haki za binadamu za kuishi na kupata chakula bora pamoja na kuboresha afya na ustawi wa mama na mtoto.
Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na utoaji Elimu ya unyonyeshaji, namna ya kuandaa uji wa mtoto na upimaji wa hali ya lishe.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.