Tuesday 3rd, December 2024
@UWANJA WA JITEGEMEE
Siku kuu ya wafanyakazi duniani hufanyika kila ifikapo Mei 01, ya kila Mwaka duniani kote ambapo wafanyakazi hupata fursa ya kuwasilisha changamoto zao kwa mwajiri ili ziweze kupata ufumbuzi ikiwa ni pamoja na suala la upandaji wa madaraja na ongezeko la Mishahara.
Kauli mbiu ya sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi ) Mwaka huu ni “MASLAHI BORA, MISHAHARA JUU, KAZI IENDELEE”
Maadhimisho ya Mei Mosi ya Mwaka 2021 kiwilaya yatafanyika katika Uwanja wa JITEGEMEE uliopo katika kitongoji cha Tanganyika kata ya Tanganyika Wilayani Muheza kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Mgeni rasmi katika Hafla hii atakuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe, Mhandisi Mwanasha Rajabu Tumbo amabaye ataongoza sherehe hizi .
Sherehe hizi zitaanza kwa maandamano kuanzia BOMANI yaani Ofisi za Halmashauri ya Wilaya Muheza na kuelekea Uwanja wa Jitegemee ambako shughuli mbali mbali za burudani na utoaji zawadi kwa wafanyakazi hodari zitafanyika.
Shime wafanyakazi wote fika , jitegemee mapema ukazungumze na mwajiri
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.