Thursday 21st, November 2024
@KWEMHOSI
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika hufanyika Juni 16 ya kila mwaka, ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine ya umoja wa Afrika kufanya kumbukizi ya mauaji ya watoto takribani 2,000 yaliyofanywa na utawala wa makaburu katika kitongoji cha SOWETO nchini Afrika kusini.
Mauaji hayo yalifanyika wakati wa maandamano ya wanafunzi waliokuwa wanapinga mfumo wa elimu ya kibaguzi iliyokuwa inatolewa na utawala wa Afrika kusini Mwaka 1991, viongozi wa Nchi za Afrika walifanya uamuzi wa kuenzi siku hiyo.
Mwaka huu 2021 maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wilayani Muheza yatafanyika katika kijiji cha KWEMHOSI kata ya NKUMBA kuanzia saa 4:00 asubuhi yatakayoongozwa na maandamano ya wanafunzi na wananchi wote watakaoshiriki shiriki siku hiyo.
Kaulimbiu ya mwaka huu “Tutekeleze ajenda 2040:kwa Afrika inayolinda Haki za Mtoto” ambayo ina lengo la kuwakumbusha wasimamizi wa sera na sheria, wazazi/ walezi na jamii yote kuhusu wajibu wao katika kulinda na kusimamia haki za mtoto.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.