Thursday 21st, November 2024
@
Maadhimisha ya siku ya Mtoto wa Afrika hufanyika kila Mwaka mnamo tarehe 16/6. Kwa Mwaka 2020 Maadhimisho haya huongozwa na kauli mbiu isemayo “Mifumo rahisi ya upatikanaji wa haki ya mtoto: Ni msingi imara wa kulinda haki zao” Ikisisitiza kuweka mifumo madhubuti na rafiki ya kushughulikia mashauri ya watoto na Changamoto nyingine zinazochangia watoto waliokinzana na sheria uendeshwaji wa makao ya marekebisho ya tabia za watoto waliopata hukumu, taratibu za kuasili mtoto, utoaji wa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya watoto, utoaji wa ushahidi mahakamani na utekelezaji na usimamizi wa sheria ya mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009.
Kutokana na kauli mbiu hii jamii inatakiwa kusimamia na kuzingatia haki ya Mtoto ya kuishi, kuhakikisha watoto wote wanapata haki ya kuendelezwa kielimu, utoaji wa haki na ulinzi wa mtoto, na kusisitiza haki ya kushiriki na kushirikishwa kwa mtoto.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.