Tuesday 3rd, December 2024
@CWT
Maadhimisho ya siku ya familia duniani hufanyika kila tarehe 15/5 ya kila Mwaka ikiwa lengo ni kujadili nafasi ya familia katika Malezi na Makuzi bora kwa watoto na changamoto zilizopo ili kuweza kuzipatia ufumbuzi.
Sherehe za Madhimisho ya siku ya Familia duniani wilayani Muheza zitafanyika siku ya Alhamisi tarehe 19/5/2022 kuanzia saa 2:00 asubuhi katika Ukumbi wa CWT.
Hafla hii itafanyika kwa njia ya mdahalo utakaoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Bulembo ambaye atakuwa ni mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Katika Mdahalo huo Mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo Saikolojia ya Malezi ya watoto, Ulinzi na Usalama wa watoto, ukatili wa kijinsia, Nafasi ya familia katika malezi na makuzi ya watoto na Uwezeshaji wa kiuchumi kwa familia katika kuboresha malezi na makuzi ya watoto.
Kaulimbiu ya Mwaka huu ni “Dumisha Amani na Upendo kwa familia imara: Tujitokeze kuhesabiwa”.
“WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA”
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.