Monday 14th, October 2024
@MAHAKAMA YA WILAYA YA MUHEZA MBARAMO
MAADHIMISHO YA KILELE CHA SHERIA
Wiki ya sheria huadhimishwa kila mwaka kuanzia Januari 22 na kilele hufanyika Mwanzoni mwa Mwezi Februari ikiwa lengo ni kutoa Elimu ya Kisheria kwa kutumia majukwaa na Mikutano mbali mbali ya wananchi ili kutatua Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi badala ya kwenda Mahakamani ambapo mara nyingi wananchi wamekuwa waki imekuwa ikitumia muda mwingi kutafuta haki hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha uzalishaji mali.
Kwa Mwaka huu wa 2023, Madhimisho ya Wiki ya Kisheria yalizinduliwa rasmi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Abdallah Bulembo siku ya Jumapili tarehe 22, 2023 katika Eneo la Stendi ya Bombani lililopo katika Kitongoji cha Tanganyika kata ya Tanganyika Wilayani Muheza.
Kilele cha Maadhimisho haya kitafanyika siku ya Jumatano Februari 1, 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Muheza Kuanzia saa 3;00 asubuhi ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Juma Irando.
Kaulimbiu ya Maadhimisho ya wiki ya Sheria kwa Mwaka huu wa 2023 inasema "Utatuzi wa Migogoro kwa Njia ya Usuluhishi katika kukuza uchumi Endelevu wajibu wa Mahakama na Wadau"
Wananchi wote mnakaribishwa.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.