Thursday 21st, November 2024
@OFISI YA MKURUGENZI
Kikao cha kamati ya Wataalam kilichofanyika jumatatu tarehe 20/5/2019 katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza Ndugu Nassib Mmbagga kilizungumzia masuala mbali mbali yaliyofanyika wiki iliopita kuanzia tarehe 13/5/2019 hadi 17/5/2019.
Kikao hicho cha Wakuu wa Idara na Vitengo kilijadili kuhusu Mapato yaliyokusanywa kwa kipindi hicho cha tarehe 13/5/2019 hadi tarehe 17/5/2019 ambapo kiasi cha TZS 20,251,103.30( zaidi ya milioni 20)
Pia Mkurugenzi mtendaji wilaya alizungumzia kuhusu maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa, wakuu wa wilaya, Makatibu Tawala Mikoa na wilaya na Wakurugenzi kilichofanyika kuanzia tarehe 16/5/2019. Ambapo miongoni mwa maagizo hayo ilikuwa ni kuhakikisha kila mmoja anawajibika ipasavyo katika idara au kitengo chake pia kuangalia kama pesa ya usimamizi wa Mradi wa TASAF 111 ya Wakuu wa Wilaya iko katika akaunti ya Halmashauri.
Kwa upande mwingine ilizungumziwa kuhusu ukarabati wa soko la mbogamboga lililopo Muheza mjini katika kata ya Tanganyika ambapo kiasi cha TZS milioni 50 kimetengwa katika bajeti ya mwaka 2019/2020
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.