Saturday 23rd, November 2024
@UKUMBI WA HALMASHAURI
Waheshimiwa madiwani wakishirikiana na wakuu wa idara na vitengo wamefanya kikao cha kamati ya fedha jana tarehe 21/5/2019 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambapo masuala mbalimbali yalizungumziwa ikiwemo taarifa ya mapato na matumizi ya mwezi machi 2019 kiasi cha Shs 20,043,594,364.28 kimekusanywa kutoka kwenye vyanzo vya ndani, ruzuku na miradi ya maendeleo kuanzia Julai 2018 hadi mwezi machi 2019 na matumizi ni kiasi cha Shs 18,924,273,673.8.
Nae Afisa Elimu Msingi Pilly Maximillian alisoma Taarifa ya Mapokezi na Mchanganuo wa Matumizi ya fedha za EP4R Tsh. 504,883,451.63 , amesema Idara ya Msingi imeingiziwa kiasi cha shs 145,430,070.98, shule za msingi zimeingiziwa shs 262,500,000.00 jumla idara ya elimu msingi 407,930,070.98
Jumla ya fedha kwa idara ya Sekondari iliyoingizwa kwenye akaunti ya halmashauri ni 96,953380.65
Hivyo basi jumla kuu ni tshs 504, 883,451.63
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.