Thursday 21st, November 2024
@Ukumbi wa Halmashauri
Kikao cha kamati ya Afya ya msingi ya kimefanyika leo Tarehe 31/5/2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri baada ya kuona ongezeko la vifo vya wakina mama wajawazito ili kuweka mikakati ya kupunguza vifo hivyo. Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa ni Mkuu wa wilaya Muheza Mhe Mwanasha Rajab Tumbo.
Katika kupunguza vifo vya wakina mama wajawazito wilayani Muheza wana kamati wameweka mikakati ifuatayo.
Pia yalizungumziwa masuala ya Lishe na mwisoni kulitolewa Tangazo la utoaji matone ya vitamin A na dawa za minyoo itakayotolewa katika vituo vyote vywa kutolea huduma kuanzia Tarehe 3/6/2019 hadi 30/6/2019 ambapo watoto kuanzia miezi 6 hadi watoto chini ya miaka 5 watahusika.
Kwa upande Mwingine Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Mwanasha Rajab Tumbo amekabidhiwa Hundi ya Milioni 5 na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya NIMR kwa ajili ya kusaidia katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza uliopo Katika kata ya Lusanga.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.