Thursday 21st, November 2024
@UWANJA WA JITEGEMEE
MKUU WA WILAYA YA MUHEZA ANAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA WILAYA YA MUHEZA KUWA MWENGE WA UHURU UTAWASILI KATIKA WILAYA YA MUHEZA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 28/5/2022 SAA 1:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA MISOZWE NA UTAKIMBIZWA UMBALI WA KILOMITA 106.
MWENGE WA UHURU WA MWAKA HUU 2022 UTAKAGUA, UTAFUNGUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MIRADI 8 YA MAENDELEO YA BARABARA YA MKUMBI –MUHEZA ESTATE KILOMITA MOJA KIWANGO CHA LAMI.
UFUNGUZI WA VYUMBA VITATU (3) VYA MADARASA YA UVIKO-19 NA UMALIZIAJI WA VYUMBA 4 VYA MADARASA SHULE YA SEKONDARI CHIEF MANG’ENYA VINAVYOTOKANA NA TOZO ZA MIAMALA YA SIMU
UWEKAJI JIWE LA MSINGI NYUMBA 4 ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MISOZWE ZILIZOPO KATIKA KIJIJ CHA MISOZWE KATA YA MISOZWE WILAYANI MUHEZA
UKAGUZI WA MRADI WA UWEZESHAJI VIJANA KIUCHUMI KIKUNDI CHA MKONGE KWANZA KINACHOJISHUGHULISHA NA BIASHARA YA UUZAJI WA ZAO LA MKONGE KILICHOPO KATIKA KITONGOJI CHA KWEMKABALA KATA YA KWEMKABALA.
UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI UKUMBI WA BURUDANI MUHEZA COMFORT ULIOPO KATIKA KITONGOJI CHA MBARAMO KATA YA MBARAMO
UFUNGUZI WA NYUMBA YA WATUMISHI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA ILIYOPO KATIKA KIJIJI CHA TANGANYIKA KATA YA LUSANGA.
KUKABIDHI VITI MEZA NA KABATI SHULE YA MSINGI MBARAMO KWENYE SHULE YA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM ILIYOPO KATIKA KITONGOJI CHA MBARAMO KATA YA MBARAMO.
NA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA MAJI MIZEMBWE ULIOPO KATIKA KIJIJI CHA PANGAMLIMA KATA YA MBARAMO, MIRADI YOTE HII IMEGHARIMU ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MOJA.
ENEO LA MKESHA, MWENGE WA UHURU MWAKA 2022 UTAKESHA KATIKA UWANJA WA JITEGEMEE.
“WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA KUSHIRIKI PAMOJA KUULAKI, KUUSHANGILIA NA KUSIKILIZA UJUMBE WA MWENGE WA UHURU MWAKA 2022”
KAULIMBIU YA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MWAKA 2022 INASEMA “SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO SHIRIKI KUHESABIWA TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA”
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.