Tuesday 3rd, December 2024
@UWANJA WA JITEGEMEE
Ibada maalum ya kuliombea Taifa na Hayati DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI itafanyika kesho ijumaa tarehe 26/3/2021 kuanzia saa 1:30 asubuhikatika Uwanja wa Jitegemee uliopo katika kitongoji cha Tanganyika kata ya Tanganyika Muheza mjini.
Katika ibada hiyo kutakuwa na Dua, Sala itakayoongozwa na Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini yaliyopo Wilayani Muheza pamoja na nyimbo za maombolezo zitakazoimbwa na vikundi mbalimbali vya sanaa.
Kadhalika kutakuwa na wimbo wa halaiki utakaongozwa na wanafunzi 200 na walimu 14 wa shule 8 za Msingi zilizopo wilayani humo.
Pia kutakuwa na zoezi la kusaini kitabu cha kumbukumbu kitakachowahusisha watu wote watakaoshiriki katika maombi hayo.
Aidha kutakuwa na Runinga (TV screen) itakayotumika mara baada ya shughuli za maombi kuisha itakayoonyesha MUBASHARA (LIVE)tukio la mazishi ya MPENDWA WETU aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati DKT JOHN POMBE MAGUFULI nyumbani kwao CHATO.
“ Pumzika kwa Amani shujaa wa Afrika”
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.