Thursday 21st, November 2024
@HOSPITALI YA WILAYA MUHEZA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Muheza anawatangazia wananchi wote kuwa siku ya jumatano tarehe 29/4/2021 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri kutakuwa na zoezi la upimaji na matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyopo katika kijiji cha Tanganyika kata ya lusanga.
Huduma ambazo zitakazotolewa ni Shindikizo la damu, uzito wa Mwili, ugonjwa wa Sukari pamoja na Ushauri nasaha juu ya kuepukana na Magonjwa yasiyoambukiza kutoka kwa Wataalamu wa Afya.
Aidha katika zoezi hilo Gharama za matibabu zitakuwa ni zakuchangia ambapo Mteja asiekuwa na kadi ya bima ya afya ya CHF na NHIF atatakiwa kuchangia fedha taslimu hivyo Mteja mwenye Kadi ya bima ya Afya atakatikiwa kufika na Kadi yake ilikuepusha usumbufu ambao unaweza kujitokeza wakati wa kupatiwa matibabu hayo.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.