Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza amepokea kibali cha Ajira mbadala cha kuajiri nafasi 02 za ajira ya kudumu za Watendaji wa Kijiji III toka kwa Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb.Na FA.170/369/01/”A”/36 cha tarehe 31/03/2020 hivyo anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba nafasi ya kazi.
MTENDAJI WA KIJIJI III (NAFASI 02)
1.Sifa za Muombaji:-
1.1. Wenye elimu ya kidato cha nne (IV) au kidato cha sita (VI)
1.2. Awe aliyehitimu mafunzo ya Astashahada /Cheti katika mojawapo ya fani zifuatazo;-
Utawala,Sheria,Elimu ya Jamii,Usimamizi wa Fedha,Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo,Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
1.3. Awe na umri usiozidi miaka 45
2. Masharti ya Jumla kwa waombaji
(a)Mwombaji awe Mtanzania
(b)Asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai
(c)Asiwe amewahi kufukuzwa kazi Serikalini
(d)Maombi yote yaambatanishwe na maelezo binafsi ya mwombaji (CV) na wadhamini wawili na
namba zao za simu
(e)Maombi yote yaambatanishwe na vivuli vya vyeti vya kuhitimu.
(g)Maombi yawe na anuani kamili pamoja na namba za simu ili kurahisisha mawasiliano
(h)Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 18/05/2020 saa 09.30 alasiri
(i)Waombaji wenye sifa wataitwa kwenye usaili
(j)Mwombaji ni lazima awe Raia wa Kitanzania.
(k)Kwa waombaji waliokuwa kazini maombi yao LAZIMA yapitie kwa Waajiri wao.
Kazi na Majukumu ya Mtendaji wa Kijiji III:-
(a)Kukusanya mapato ya Kijiji na Halmashauri.
(b)Kusimamia Ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao,kuwa mlinzi wa Amani na Msimamizi wa
Utawala Bora katika Kijiji.
(c)Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Kijiji.
(d)Katibu wa Mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
(e)Kuandaa taarifa za utekelezaji na kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuunda
na kutekeleza mikakati ya kuondoa umasikini na ujinga na maradhi.
(f)Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika Kijiji
(g)Mwenyekiti wa Kikao cha wataalam waliopo katika kikao
(h)Kusimamia utungaji na utekelezaji wa sheria ndogo za Kijiji
Ngazi ya Mshahara
Ngazi ya Mshahara kwa cheo hiki ni Tshs. TGS. B1 390,000/= kwa mwezi.
Maombi yote yatumwe kwa:-
MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA,
HALMASHAURI YA WILAYA,
S.L.P 20,
MUHEZA.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.