Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe Mwanasha Rajab Tumbo amewataka wazazi kutenga muda kuongea na watoto wa ili waweze kufahamu mambo mbalimbali wanayokumbana nao pindi wawapo Shuleni na Mitaani.
Akizungumza katika Sherehe za Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika jana tarehe 8/3/2020 katika uwanja wa Jitegemee Mhe Mwanasha amesema watoto wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili kama ubakaji , ulawiti hivyo basi wazazi wawe imara kusimamia watoto wao ili kuhakikisha wanasoma vyema na kuweza kuisaidia nchi hapo baadae.
”tuwasikilze watoto wetu wawe wa kike au kiume kwani mara nyingi wamekuwa wakibakwa na kulawitiwa mara kwa mara wanapokuwa shuleni na majumbani na wengine hufanyiwa vitendo hivi na ndugu zetu , watoto wenzao na waume zetu, wageni wanaokuja majumbani mwetu tuhakikishe tunawasimamia vyema ili waweze kufikia malengo yao ya kuhudumia Nchi hii ya Tanzania” alisema Mhe Tumbo.
Sambamba na hayo amewataka wanawake kupendana na kusaidiana pindi wa patapo matatizo badala ya kuleteana maneno ya fitna, Majungu na uongo ili kuleta tija na maendeleo katika taifa kwani wao ndio chanzo kikubwa cha kuinua uchumi wa Taifa
“Ndugu zangu nataka niwaaminishe kuwa uchumi wa nchi hii unaongozwa na wanawake , hivyo basi tupendane, na kusiadiana pale unapoona mwenzako ana nafasi fulani usipeleke maneno ya fitna wala majungu, anapokosea mwenzako msahihishe na msaidie. alisema Mkuu wa Wilaya Muheza.
Aliongeza kuwa wanawake wajiunge katika vikundi vya ujasiriamali ili waweze kupatiwa mikopo na waweze kuongeza kipato cha kaya kwani Halmashuri ikupitia mapato yake ya ndani hutenga 10% kila mwaka kwa ajili ya kukopesha vijana asilimia 4, wanawake asilimia 4 wanawake na wenye ulemavu asilimia 2 hivyo wanawake wachangamkie fursa hii na wahakikishe wanarejesha kwa wakati.
Vile vile amewataka wanawake wanapopata matatizo wapeleke migogoro yao kwenye vyombo vya kisheria kama vile kwenye madawati ya jinsia yaliyopo polisi ambako haki na usawa wa mwanamke huzungumziwa .
Kwa upande mwingine ameitaka jamii kuepukana na tabia ya kushikana mikono pindi wasalimianapo, kukumbatiana, kubusiana na kuwataka wanawe mikono mara kwa mara ikiwa ni tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa korona ambao mpaka sasa umeua watu wengi Nchini China.
Awali akisoma Risala kwa mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajabu , Diwani viti maalum kata ya Amani Mhe Mariamu Nyota amesema tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanafanya kazi nyingi kwa saa 16 hadi 18 kwa siku ikiwa na maana kwamba wana saa 6 hadi 8 tu za kulala, kupumzika na kushiriki shughuli nyingine hali inayosababishwa na mila na desturi zilizojengeka katika jamii hali hii husababisha wanawake kubebeshwa mzigo mzito wa majukumu hali inayowafanya wakose muda wa kujiendeleza.
Aliongeza kuwa baadhi ya mila na desturi potofu huvunja haki za mwanamke kama tabia za ukeketaji wa watoto wa kike kuwanyima wanawake haki ya kurithi mali ya marehemu mume wake, kuwanyima haki ya kupata elimu, kuwaozesha katika umri mdogo, kuwanyima haki ya kumiliki ardhi ni baadhi ya mifano michache ya ukiukwaji mkubwa wa haki za wanawake kwa kisingizio cha Mila na Desturi.
Aliendelea kuwa baadhi ya wanawake hufanyiwa vitendo vya ukatili wa kimwili au kingono na wenza wao na hivyo kuathiri maendeleo yao ya kiafya, kisaikolojia na kiuchumi.
Akiitaja kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na baadaye” ameishukuru Serikali kwa jitihada zake za kujenga usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume kwa kuwawezesha kupata mikopokutoka Halmashauri yenye asilimia sawa na wanaume pia kwa kuanzisha majukwaa yanayolenga kusimamia usawa wa wanawake na wanaume
Aidha siku ya wanawake duniani iliadhimishwa kwa kuandamana toka bomani mpaka Uwanja wa Jitegemee, upimaji wa HIV, ushauri nasaha, ukaguaji wa mabanda ya wajasiriamali, mashindano ya kukimbiza kuku, kuvuta kamba na kucheza mpira wa miguu baina ya wanawake wa Tarafa ya Muheza na Tarafa ya Amani sanjari na hafla ya usiku wa Mwanamke uliofanyika katika ukumbi wa TARECU ambako maonyesho ya Mavazi ya tamaduni mbali mbali yalionyeshwa.
WANAWAKE WAKIWA KWENYE MAANDAMANO | MHE, DIWANI VITI MAALUM KATA YA AMANI MARIAM NYOTA AKISOMA RISALA KWA MGENI RASMI |
|
|
||
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.