Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mhandisi Mwanasha Tumbo amepiga marufuku vitendo vya uwekezaji wa mazao ya viungo vinavyofanywa na wananchi wa Muheza wenye mashamba yanayolima mazao hayo ili yaweze kuwa chachu ya maendeleo katika maisha yao.
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha jukwaa la mazao ya viungo lililofanyika siku ya jumanne tarehe 17/11/2020 katika ukumbi wa MCHINA uliopo katika kata ya Nkumba ambacho kilijumuisha wadau mbalimbali wa mazao.
Jukwaa hilo lilihudhuriwa na wataalam kutoka makao makuu wilaya, watendaji kata, watendaji vijiji, maafisa ugani, wanunuzi wa mazao ya viungo(wafanyabiashara), viongozi wa mashirika au taasisi zinazojishughulisha na mazao ya viungo , kamati ya ulinzi na usalam na wakulima.
Akizungumza katika jukwaa hilo Mhe, Mwanasha amesema ni marufuku kwa Mkulima yeyote kuuza au kuwekeza mazao machanga ambayo hayajakomaa kwa kuuza kwa mfanyabiashara au mtu yeyote atakayebainika ametenda kosa hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Akiwataka wakulima wafuate kanuni na taratibu za serikali Mkuu wa Wilaya amemtaka Mwanasheria kuhakikisha sheria ndogo za kilimo cha uvunaji wa mazao hayo inaandaliwa haraka iwezekanavyo ili watakaovunja sheria wachukuliwe hatua.
Kwa upande wake Afisa kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Wilaya Muheza Hoyange Mbwambo Marika amewataka wadau wa kilimo kujisajili na kuuliza maswali kwa kutumia namba hi 0689666662 ili waweze kutatuliwa changamoto zinazowasumbua.
Nae Mwenyekiti wa jukwaa la viungo ambaye ni MTendaji kata ya Kisiwani Bw. AYUBU MHINA aliwataka wadau hao wapange tarehe ya uvunaji wa mazao ya viungo, ikatakwa kwamba Potwe Nkumba na Tongwe wataanza kuvuna pilipilimanga mnamo Januari , 20/12/2020 na kwa ukanda wa Magoroto uvunaji utaanza tarehe 15/1/2021. Ikiwa ukanda wa Amani uvunaji ulishaanza
Aidha Uzinduzi wa uvunaji wa Mazao haya ya viungo utafanyika mnamo tarehe 20/12/2020 katika kijiji cha Ubembe kata ya Nkumba, wananchi wametakiwa kuhudhuria kwa wingi ili kufanikisha zoezi hili.
MKUU WA WILAYA MUHEZA MHE, MWANASHA TUMBO AKIZUNGUMZA WAKATI WA JUKWAA LA WADAU WA VIUNGO | AFISA KILIMO USHIRIKA NA UMWAGILIAJI WILAYA AMBAYE NI KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WILAYA MUHEZA(KULIA) BW. HOYANGE MBWAMBO MARIKA AKIWA NA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WADAU WA VIUNGO AMBAYE PIA NI AFISA MTENDAJI KATA YA KISIWA NI AYUBU MHINA (KUSHOTO) WAKISILIZA TAARIFA MBALIMBALI ZILIZOKUWA ZIKIWASILISHWA | WADAU WA JUKWAA WAKIWASILISHA TAARIFA MBALIMBALI ZA MAZAO YA VIUNGO | SEHEMU YA WATAALAMU WALIOSHIRIKI KATIKA JUKWAA LA WADAU WA VIUNGO TAREHE 17/11/2020 KATIKA UKUMBI WA MCHINA - NKUMBA | SEHEMU YA WADAU MBALIMBALI WALIOSHIRIKI KATIKA JUKWAA LA VIUNGO TAREHE 17/11/2020, WAKULIMA, WATENDAJI KATA, WATENDAJI VIJIJI, MAAFISA UGANI, |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.