11.0 TAARIFA YA MRADI WA UKAMILISHAJI WA MADARASA MATUTU NA OFISI PAMOJA NA UJENZI WA VYOO MATUNDU TISA
SULE YA MSINGI NGARANI 2025/2026
11.1 UTANGULIZI.
Shule ya msingi Ngarani ipo kata ya Kwakifua, Tarafa ya Muheza, shule inajumla ya wanafunzi 632 kati yao wavulana 314 na wasichana 318. Shule ina jumla ya walimu 9 kati yao me 2 na ke 7. Pia shule ina kituo shikizi kilichopo Kijiji cha Mpakani shule hii iliingiziwa fedha za mradi wa ukamilishaji wa vyumba vitatu (3) vya madarasa na ofisi. Pia ujenzi wa vyoo matundu tisa (9) kutoka mradi wa Boost wenye thamani ya jumla ya sh. 58,900,000/=
Ujenzi huu ulianza tarehe 31/10/2025 kwa mkataba wa miezi 3 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30/01/2026.
11.2 HALI YA MRADI.
Hali ya miradi yote miwili yaani mradi wa ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na ofisi na ujenzi wa vyoo matundu tisa (9) ni kama ifuatavyo:-
Mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mradi huu upo hatua za mwisho za umaliziaji zikiwemo upakaji wa rangi na ukamilishaji wa sakafu ambapo tunasubiri tiles kutoka kwa mzabuni.
Mradi wa matundu tisa (9) ya vyoo:-
Mradi huu uko katika hatua ya ukamilishaji na usafi uwekaji wa sakafu. Na umekamilika kwa asilimia 90.
11.3 GHARAMA ZA MRADI.
|
KIASI KILICHOPOKELEWA |
KIASI KILICHOTUMIKA |
KIASI KILICHOBAKI |
|
| BOOST
|
58,900,000/= |
47,752,750.00 |
11,147,250.0 |
| Nguvu za wananchi
|
22,589,240/= |
22,589,240.00 |
- |
| Mfuko wa jimbo
|
Saruji 15 Tshs.225,000/=
|
225,000.00 |
- |
| JUMLA
|
59,125,000
|
70,566,990 |
11,147,250 |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.