2.0 TAARIFA YA MIRADI UJENZI WA JENGO LA KARAKANA NA MATUNDU 02 YA VYOO SHULE YA MSINGI NA UFUNDI MAGILA
2.1 Utangulizi
Shule ya msingi Magila ipo Kata ya Magila, tarafa ya Muheza, shule hii ina jumla ya wanafunzi 397 kati yao wavulana 184 na wasichana 213 na walimu 12 me 5 na ke 7 pia kufuatia muongozo tuliopewa tumeshafanya usajili wa wanafunzi tarajali wa mafunzo ya ufundi 82 me 25 na ke 57 na usajili bado unaendelea.Shule hii ya ufundi ina jumla ya Walimu 5 kati yao me 2 na ke 3 ambao ni miongoni mwa walimu 12 waliotajwa hapo juu.
Shule hii iliingiziwa fedha za mradi wa ujenzi wa jengo la karakana na matundu mawili ya vyoo vyenye thamani ya jumla ya Sh. 54,000,000/= Kutoka Serikali kuu kupitia Mhisani COICA ambapo fedha hiyo iliingizwa kwa awamu mbili awamu ya kwanza ambayo iliingizwa Sh. 27,000,000/=, na awamu ya pili iliingizwa Sh. 27,000,000/=. Ujenzi huu ulianza rasmi mnamo tarehe 08/05/2025 kwa mkataba wa siku 60 hivyo unatarajiwa kukamilika tarehe 08/07/2025.
2.2 HALI YA MRADI
Hali ya mradi kwa sasa tumeweza kutekeleza ujenzi huu kwa maeneo yote mawili kama ifuatavyo;-
Mradi wa jengo la karakana; Mradi huu uko kwenye hatua za mwisho za umaliziaji ambapo ujenzi umekamilika kwa 98%.
Mradi wa matundu mawili ya choo; Mradi huu uko kwenye hatua ya upigaji wa ripu na ujenzi wa lampu na ngazi ambapo ujenzi umekamilika kwa 85%.
2.3 GHARAMA ZA MRADI
Gharama ya mradi huu ni kama ifuatavyo;-
A.Ujenzi wa jengo la karakana na matundu 2 ya vyoo
Gharama iliyotumika hadi sasa katika ujenzi wa jengo la karakana na matundu 2 ya vyoo ni kama ifuatavyo:-
|
CHANZO CHA FEDHA |
FEDHA POKELEWA |
ZILIZOTUMIKA |
SALIO BANK |
|
COICA |
54,000,000.00 |
53,105,777.00 |
894,223.00 |
|
DED MUHEZA |
1,600,000.00 |
1,600,000.00 |
0 |
|
WANANCHI |
120,000.00 |
120,000.00 |
0 |
|
JUMLA KUU |
55,720,000.00 |
54,825,777.00 |
894,223.00 |
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.