Mkuu wa Mkoa Tanga, Mhe Martin Shigella amefanya Ziara katika Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Muheza uliopo katika kata ya Lusanga Tarafa Ngomeni leo tarehe 11/04/2019 ili kujiridhisha na utekeleza wa hatua uliofikia Mradi huo .
Akifurahishwa na jitihada za ujenzi wa hospitali huo Mhe shigella amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Muheza kwa kusimamia vyema ujenzi wa majengo 8 ambayo ni ,Jengo la utawala, jengo la wagonjwa wa nje, jengo la upasuaji, jengo la kufulia, jengo la watoto,jengo la wakina mama, na jengo la kuhifadhia dawa ya Hospitali hiyo ambayo mpaka sasa yako katika hatua nzuri na kuwataka waendelee kusimamia kwa karibu ili ifikapo Tarehe 30/6/2019 ujenzi uwe umekamilika.
Aidha amewataka kuongeza nguvu katika majengo ambayo yako katika hatua ya chini ili yaweze kuendana na kasi ya mradi na kuweza kutimiza lengo la Serikali la kuhakikisha majengo yote yanakamilika juni mwaka huu.
Pia alitoa rai kwa viongozi hao kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinapatikana muda wote na kuahidi kutembelea mara mara katika ujenzi huo ili kuhakikisha kuwa maagizo aliyoyatoa yametekelezwa na ujenzi unaendelea vizuri
Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella akishirikiana na kamati ya Ulinzi na Usalama na wataalam wa Wilaya Muheza wakikagua Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
|
|
Mkuu wa Wilaya Muheza Mhe, Mwanasha Rajabu Tumbo (mwenye nguo nyeusi) akiteta jambo na wahe madiwani viti Maalum Tarafa wakimsubiri mkuu wa mkoa. |
---|---|---|
|
||
|
||
|
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.