Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ilipokea fedha kiasi cha Shilingi Milioni tisini (90) kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kujenga Nyumba za watumishi (3in 1) katika Hospitali ya Wilaya ya Muheza iliyopo katika kijiji cha Tanganyika kata ya Lusanga,
Lengo kuu la kujengwa nyumba hizo katika Hospitali hiyo ni kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka zaidi mara baada ya wagonjwa kuwasili katika Hospitali hiyo lakini pia kupunguza idadi ya vifo kwa wagonjwa.
Mpaka sasa ujenzi huu umekamilika na taratibu za kuwapeleka watumishi wa afya katika nyumba hizi unaendelea , tuaishukuru Serikali awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Samia Suluhu Hassan kwa usikivu na kuwaspgezea karibu huduma huduma ya afya wananchi wa Muheza.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.