Mbunge wa Jimbo la Muheza Hamisi Mwinjuma (MWANA FA) amewataka wananchi amabao bado hawajahesabiwa mara watakapofikiwa na karani wa sensa watoe taafifa sahihi za wanakaya wote waliolala kwenye kaya zao usiku wa kuamkia siku ya sensa ili lengo la Serikali la kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake liweze kufanikiwa inapopanga ifanikiwe kwa asilimia kubwa.
Ameyasema hayo jana tarehe 23/8/2022 mara baada ya kuhesabiwa katika kijiji cha Kwemhanya kilichopo katika kata ya Kilulu Wilayani Muheza.
“Hakikisheni mnatoa ushirikiano wa kutosha kwa karani wa sensa kwa kutoa taarifa sahihi za kaya zenu ili kuweza kufikia adhima ya Serikali yenye lengo la kuliletea maendeleo Taifa letula Tanzania, “ alisema Mbunge wa jimbo la Muheza
SENSA KWA MAENDELEO JIANDAE KUHESABIWA, JITOKEZE KUHESABIWA KWA MAENDELEO YA TAIFA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.