BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA SHS BIL. 48
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Muheza likiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Salimu Sechambo limepitisha kwa kishindo Bajeti ya Mwaka 2026/2027 Shilingi Bilioni arobaini na nane mlilioni mia saba hamsini na tatu laki nane na elfu thelathini na Saba (48,753,837,000) ambazo ni Ruzuku kutoka Serikali Kuu na makusanyo yatokanayo na Vyanzo vyake vya ndani.
Baraza hilo la Madiwani lililoketi tarehe 23/1/2026 limepitisha na kukubaliana kwa pamoja kuwa kiasi kilichopangwa kikatumike kama kilivyopangwa kisha walimsisitiza Mkurugenzi wa Halmasjhauri hiyo kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya miradi zinapelekwa ipasavyo na kuhakikisha usimamizi wa karibu wa Miradi ya maendeleo ili iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa.
Akizungumza kwa msisitizo Mwenyekiti huyo wa Halmashauri amesema Baraza lake halitomvumili mtu yeyote atakaeshindwa kusimamia kikamilifu Miradi ya maendeleo na atakaeonesha dhamira mbaya ya kuchezea vyanzo vya Mapato.
“Niseme ukweli kwa dhati ya Moyo wangu kuwa hatutamuonea mtu lakini pia hatutamfumbia macho mtu yeyote mwenye nia ovu ya kutaka kukwamisha maendeleo ya Halmashauri na ikitokea hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya mtu huyo” alisistiza Mhe.Sechambo.
Awali akiwasilisha taarifa ya umbile la bajeti kwa Mwaka wa fedha 2026/2027 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza Dkt Jumaa Mhina, Afisa Mipango wa Halmashauri Bi. Mwanaisha Dallah amesema Halmashauri ya Wilaya ya Muheza imekisia kupokea ruzuku kutoka Serikali kuu na kukusanya mapato ya ndani kutoka vyanzo vyake Jumla ya Sh. 48,753,837,000/=.
Amefafanua kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 32,831,352,000/= Malipo ya Mishahara, ikiwa Shilingi 1,924,838,000/= ni fedha za Matumizi Mengineyo, ambapo Shilingi 9,738,618,000/= zitapelekwa kwenye Miradi ya Maendeleo na kiasi kilichosalia cha Shilingi 4,259,034,000/= kitakusanywa kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.