Thursday 21st, November 2024
@MASUGURU
Maadhimisho ya Wiki ya Msada wa Sheria hufanyika Novemba, 12 hadi Novemba 18 ya kila Mwaka.ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa viongozi wanaosimamia kero za wananchi ili waweze kuzitatua lakini pia waweze kutenda haki kwa wananchi.
Kwa Mwaka 2020 Maadhimisho ya Wiki ya sheria Wilayani Muheza yatafanyika kwa Muda wa siku 3 kuanzia jumanne tarehe 17/11/2020 hadi Alhamisi tarehe 19/11/2020 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika eneo la samaki la soko la samaki la zamani (MSIKITI MKUBWA) lililopo katika Kitongoji cha Uhuru kata ya Masuguru.
Shughuli zitakazofanyika kwa siku zote 3 ni kutoa elimu na Msaada wa sheria ya Mirathi na Wosia kwa kuwa Malalamiko ya wananchi wengi yamejikita katika maeneo hayo, Iwapo Kauli mbiu ya Mwaka huu ni “USIMAMIZI BORA WA MIRATHI KWA MAENDELEO YA FAMILIA”.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.