Thursday 21st, November 2024
@kijiji cha Bombani kata ya Tongwe
Mfuko wa Afya wa jamii ulioboreshwa unatoa fursa kwa kaya moja yenye watu wasiozidi sita (6) kupata matibabu katika Zahanati, kituo cha Afya, Hospitali ya Wilaya, na Hospitali ya rufaa ya Mkoa kwa gharama ya shilingi elfu thelathini(30,000) kwa Mwaka.
Ili uweze kujiunga na huduma hii, fika katika ofisi ya kata/ kijiji au Mtaa unapoishi uweze kupata taarifa Za Afisa mwandikishaji.
Uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (ICHF) utafanyika kesho IJUMAA tarehe 25/6/2021 katika kijiji cha BOMBANI kata ya TONGWE kuanzia saa 7:00 mchana.
Mgeni rasmi katika Uzinduzi huo atakuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Halima Abdallah Bulembo ambaye ataongoza zoezi hilo.
Sanjari na Uzinduzi huo kutakuwa na huduma za upimaji wa magonjwa yasiyoambukizwa kama vile upimaji wa sukari, lishe na shinikizo la damu ambapo huduma hii itatolewa bila malipo.
Vile vile elimu ya utoaji na usajili wa vyeti kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano(5) itatolewa katika hafla hiyo.
WOTE MNAKARIBISHWA
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.