Thursday 21st, November 2024
@Kituo cha afya ubwari
Zoezi la Utoaji wa chanjo ya polio awamu ya tatu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano (5) limeanza leo siku ya Alhamisi tarehe 1/9/2022 na linatarajiwa kukamilika siku ya jumapili tarehe 4/9/2022.
Huduma hii hutolewa bure/ bila malipo kwa watoto hao ambapo wataalam wa afya watapita nyumba kwa nyumba au sehemu yeyote alipo mtoto na kwenye vituo vya kutolea huduma za Hospitali, Vituo vya afya na Zahanati.
Chanjo hii ni salama haina madhara yoyote na inatolewa kwa watoto wenye umri huu ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa wa kupooza na wanapatiwa watoto hawa hata kama walishapata chanjo hii kwenye utaratibu wa kawaida.
“Ewe mzazi au Mlezi hakikisha mwanao anapata chanjo hii ya matone ili kumkinga dhidi ya ugonjwa wa kupooz”
Mpe matone Okoa maisha
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.