Wednesday 22nd, April 2026
@KATA YA MBOMOLE
MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
Kilele cha Maadhimishoya siku ya wanawake Duniani hufanyika kila tarehe 8/3 ya kila Mwaka ikiwa ni hatua ya kutafakari masuala mbalimbali yahusuyo jinsia ya kike ikiwemo Haki ya Mwanamke kwenye jamii, wajibu wa mwanamke, na namna gani mwanamke anaweza kujikwamua kiuchumi, kijamii na kifikra.
kwa Mwaka huu wa 2026 Maadhimishoya Siku ya Wanawake Wilayani Muheza yamefanyika tarehe 4/3/2026 katika Kijiji cha Mbomole ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Ayubu Sebabili.
Hafla hiyo imefanyika mapema kupisha kilele cha maadhimisho kitakachofanyika Kimkoa Wilayani Korogwe siku ya Jumapili tarehe 8/3/2026 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Batilda Buriani atakuwa mgeni rasmi.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Mwaka huu wa 2026 yanaongozwa na kaulimbiu isemayo" Haki kwa Wanawake na wasichana msingi wa maendeleo jumuishi kufikia Dira 2050"
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.