Thursday 21st, November 2024
@nyumbani, zahanati, kituo cha afya na Hospitali
Chanjo ya matone ya polio itatolewa kwa muda wa siku 4 kuanzia siku ya jumatano tarehe 18/5/2022 hadi tarehe 21/5/2022 ambapo wataalam wa afya watapita nyumba kwa nyumba au sehemu yeyote alipo mtoto ili kumkinga dhidi ya ugonjwa wa kupooza.
Kadhalika huduma hii itatolewa bila malipo (bure) kwenye vituo vya kutolea huduma za afya Zahanati, kituo cha afya na hosipitali kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano yaani kuanzia Mwezi 0- 59, hata kama wameshapata chanjo hii kwenye utaratibu maalum wanatakiwa kuchanja tena.
Kaulimbiu ya kampeni hii inasema “Kila tone la chanjo ya polio litaiweka Tanzania salama dhidi ya Ugonjwa wa kupooza”
Chanjo hii iko salama haina madhara yoyote, Ewe Mzazi au Mlezi hakikisha mwanao anapata chanjo hii ya matone ili kumkinga dhidi ya ugonjwa wa polio
.
“MPE MATONE OKOA MAISHA”
Muheza Mjini, Bomani
Anwani ya posta: S.L.P 20 MUHEZA
Simu: 027-2977545
Simu ya Mkononi: 0746525653
Barua Pepe: ded@muhezadc.go.tz
Copyright ©2018 Muheza District Council . All rights reserved.